Lukaku atinga kifahari kwenye mazoezi - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 14 August 2018

Lukaku atinga kifahari kwenye mazoezi

Nyota wa Manchester United, Romelu Lukaku ametinga mazoezini kifahari leo siku ya Jumanne kwa kuendesha gari jipya aina ya Mercedes AMG-GT Coupe.
Lukaku ametinga Carrington na ‘brand new’ Mercedes AMG-GT Coupe nyeusi yenye thamani ya pauni 102,030 ambayo kwa fedha za Kitanzania ni sawa na milioni 297.
Mchezaji huyo raia wa Ubelgiji ambaye kwa sasa anaingiza pauni 200,000 kwa wiki baada ya mkataba mpya na United unaomuweka hadi mwaka 2022 inamchukua siku nne tu kwa gharama ya gari hilo.
Mbwembwe hizo zinakuja baada ya Manchester United kushinda kwenye mchezo wake wa kwanza ligi kuu England kwa jumla ya magoli 2 – 1 dhidi ya Leicester siku ya Ijumaa.

No comments:

Post a Comment