Liverpool yaanza ligi kibabe, Mane na Salah kama kawaida - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 12 August 2018

Liverpool yaanza ligi kibabe, Mane na Salah kama kawaida

Klabu ya Liverpool imeanza vema msimu wa ligi kuu soka England mara baada ya kuibuka na ushindi mnono wa jumla ya mabao  4 – 0 dhidi ya West Ham.
Katika mchezo huo uliyopigwa dimba la Anfield mashabiki wa soka walishuhudia Mohamed Salah akiandika bao la mapema dakika ya 19 kisha Sadio Mane akitupia mawili dakika ya (45+2) na 53 wakati Daniel Sturridge akihitimisha karamu ya magoli baada ya kufunga dakika 88 ya mchezo huo.
Kwa matokeo hayo sasa Liver inaongoza ligi kwakuwa na idadi kubwa ya magoli ukilinganisha na wapinzani wake wakubwa Man United na Man City.
Vikosi vya timu zote Liverpool: Alisson (7), Alexander-Arnold (8), Van Dijk (7), Gomez (7), Robertson (8), Keita (9), Milner (9), Wijnaldum (7), Mane (8), Salah (8), Firmino (8)
Wachezaji waakiba : Henderson (6), Shaqiri (6), Sturridge (7)
West Ham: Fabianski (7), Fredericks (6), Balbuena (6), Rice (5), Ogbonna (6), Masuaku (6), Noble (5), Wilshere (6), Anderson (7), Arnautovic (7), Antonio (6)
Wachezaji waakiba: Snodgrass (6), Hernandez (6), Yarmolenko (6)
Mchezaji bora wamchezo ni James Milner

No comments:

Post a Comment