LEWANDOWSK, HAZARD, MIGNOLET, HAZARD, ZIDANE, WILLIAN: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 1 August 2018

LEWANDOWSK, HAZARD, MIGNOLET, HAZARD, ZIDANE, WILLIAN: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO


Manchester United wanamtaka kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kuichukua nafasi ya Jose Mourinho kama meneja ikiwa Mourinho ataondoka klabu ya Old Trafford (Sun)

Inter Milan wanataka kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati wa Real Madrid Mcroatia Luka Modric, mwenye umri wa miaka 32, ambaye yuko mapumzikoni kwa sasa nchini Italia. (Mail)

Chelsea inatumai kuipiku Real kwa kusaini mkataba na mchezaji wa wa safu ya mashambulizi wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski mwenye umri wa miaka 29. (Star)

The Blues wanatumai kwa kumtoa mchezaji wa safu ya kati N'Golo Kante kwa mkataba mpya wa £290,000- wa kila wiki ikiwa wanaweza pia kumshawishi mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 27, kuendelea kubaki katika Stamford Bridge. (Evening Standard)

Hata hivyo Paris St-Germain hawakati tamaa ya kusaini mkataba na mchezaji wa kimataifa wa timu ya Ufaransa Kante alie na umri wa miaka 27. (mirror)

Chelsea bado hawajaridhishwa na kuchelewa kurejea kwa winga wa Brazil Willian kwenye klabu hiyo kwasabau ya masuala ya paspoti, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akiwa bado hajaripoti kwenye mazoezi ya kabla ya msimu . (Times - subscription required)

Mchezaji wa Liverpool mwenye umri wa miaka 30 - mlinda lango wa Ubelgiji Simon Mignolet analengwa kuchukuliwa na Barcelona. (Sky Sports)

Mchezaji wa safu ya ulinzi Luke Shaw, mwenye umri wa miaka 23, anafurahia kuuona mwaka wa mwisho wa mkataba wake katika Manchester United, licha ya klabu ya Ujerumani ya Wolfsburg kumtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa England (Mail).

Mshambuliaji wa timu ya Ubelgiji Michy Batshuayi, mwenye umri wa miaka 24, ameambiwa na meneja wa Chelsea Maurizio Sarri kwamba nafasi ijayo katika Stamford Bridge, huku Crystal Palace na Valencia wakionyesha utashi wa kumchukua .(RMC, via Sun)

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment