Klabu ya Levante Yamuhitaji Mbwana Samatta - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 1 August 2018

Klabu ya Levante Yamuhitaji Mbwana Samatta

Nyota wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya soka ya KRC Genk ya ligi kuu ya Ubelgiji Mbwana Samatta, huenda akatua kwenye ligi kuu ya soka ya Hispania kwa msimu ujao, baada ya klabu ya Levante kuonesha nia ya kuhitaji huduma yake.

Meneja wa nahodha huyo wa Taifa stars, Jamal Kasongo ameiambia www.eatv.tv kwamba yapo mazungumzo yanayoendelea kufanyika baina ya pande zote mbili na endapo yatakamilika basi huenda tukamshuhudia Samatta akivuma katika ligi bora zaidi barani Ulaya maarufu kama La Liga.

Akiwa na Genk ambayo alijiunga nayo mwaka 2016, akitokea TP Mazembe ya DRC, Samatta amecheza mechi 66 na amefanikiwa kufunga mabao 19. Tayari Samatta ameshakuwa na uzoefu wa ligi za Ulaya baada ya kucheza michuano ya Europa League msimu uliopita ambayo ni ya pili kwa ukubwa ngazi ya vilabu barani humo baada ya ligi ya Mabingwa.

www.eatv.tv tunapenda kuomba radhi uongozi mzima wa nyota huyo akiwemo meneja Jamal Kasongo na wakala wake, bila kusahau mashabiki wake pamoja na wasomaji wetu kwa taarifa tuliyoitoa ikimhusisha Samatta kutakiwa na klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani. Taarifa hiyo haikuwa sahihi bali hii ndio taarifa rasmi.

No comments:

Post a Comment