KISA SALAH, RAMOS AENDELEZA UHASAMA NA LIVERPOOL, AWAMU HII AMCHANA KLOPP - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 15 August 2018

KISA SALAH, RAMOS AENDELEZA UHASAMA NA LIVERPOOL, AWAMU HII AMCHANA KLOPP


Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos ameendeleza uhasama wake na klabu ya Liverpool uliozidishwa na kuumia kwa nyota wa Liverpool Mo Salah, wakati huu kwa kumshutumu meneja wao.

Ramos amemwambia Jurgen Klopp kwamba "baadhi yetu tumekuwa tukicheza soka katika kiwango cha hali ya juu sana kwa miaka mingi - Sina uhakika kama yeye mwenyewe anaweza kusema hivyo".

Kwa mujibu wa BBC, Klopp alimkosoa Ramos baada ya Mohammed Salah kuumia kwenye bega alipokabiliwa na beki huyo wa Real Madrid wakati wa fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi Mei.

Salah alilazimika kuondoka uwanjani kabla ya kumaliza hata kipindi cha kwanza.

Klopp alisema mchezaji huyo wa miaka 32 alikuwa "katili".

Lakini Ramos amesema: "Sina nia yoyote ya kumuumiza mchezaji makusudi."

Ameongeza: "Atakuwa anahitajika kueleza ni kwa nini hakushinda mechi hiyo ya fainali, lakini si mara yake ya kwanza kushindwa."

Klopp alishinda fainali yake ya kwanza ya michuano yoyote ile ya kiwango cha juu akiwa meneja mwaka 2012 katika Kombe la Ujerumani akiwa na Borussia Dortmund.

Lakini ameshindwa katika fainali sita alizozicheza karibuni zaidi - ikiwa ni pamoja na fainali hiyo ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid na fainali ya ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, dhidi ya Sevilla mwaka 2016.

Salah alilazimika kufanyiwa upasuaji kwenye bega baada ya kuumia uwanjani mwezi Mei.

No comments:

Post a Comment