Kimenuka...Polisi Wanaofanya Uhalifu Ndani ya Jeshi Kuuawa - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 9 August 2018

Kimenuka...Polisi Wanaofanya Uhalifu Ndani ya Jeshi KuuawaUFILIPINO: Rais Rodrigo Duterte ametishia kuwaua maofisa wa Jeshi la Polisi ambao wako chini ya uchunguzi kwa uhalifu katika hotuba iliyojaa dharau akilenga wahalifu ndani ya Jeshi hilo

Duterte, Rais mwenye maneno ya ufedhuli, Jumanne aliwashambulia maofisa wa Polisi 102 akisema 'hawana maana na ni mzigo kwa jamii'

Majina ya maofisa wengi wa Polisi yako chini ya uchunguzi kwa makosa makubwa ya uhalifu yakiwemo ya ubakaji, kuteka, kupotosha na kujihusisha katika biashara ya dawa za kulevya

Duterte aliwaonya maofisa hao kwamba ikiwa wataendelea na vitendo vyao vya uhalifu na kugundulika basi watauawa

No comments:

Post a Comment