Kamati ya Mazishi ya Mzee Majuto Yamtosa Steve Nyerere Yamnyima Uongozi Kisa Hiki Hapa - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 9 August 2018

Kamati ya Mazishi ya Mzee Majuto Yamtosa Steve Nyerere Yamnyima Uongozi Kisa Hiki Hapa

Muigizaji Steve Nyerere ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwaunganisha wasanii hasa katika kipindi cha misiba au matatizo yanayowatokea wasanii wenzao, ametoswa kwenye msiba wa Mzee Majuto.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuundwa kamati ya kushughulikia msiba huo ambayo imeundwa na Chama cha waigizaji Mkoa wa Kinondoni (TDFAA) pamoja na chama cha waigizaji Taifa.

Kuondolewa kwa Steve ni kutokana na kutokuwa mwanachama  wa TDFAA,  hivyo hawezi kuteuliwa katika kamati.

Mara baada ya Mzee Majuto kufariki, wajumbe wa kamati wakiongozwa na Simon Mwakifamba walifika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya taratibu za kuhifadhi mwili na wakatoa tamko kwamba taratibu zote za kuaga zitafanyika Muhimbili na baadaye kusafirisha kwenda Donge, jijini Tanga kwa maziko.

Wakati hayo yakiendelea Steve Nyerere alifika Muhimbili saa 6.05 usiku, akija na utaratibu mwingine kuwa shughuli za kuaga zifanyike kwenye viwanja vya Karimjee kwa kuwa Majuto ni mtu maarufu na tayari walishaanza kukaa kikao na wasanii wenzake kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kuagiwa kwenye viwanja hivyo.

Hata hivyo, alipotoa wazo hilo, mmoja wa wanandugu alijitambulisha kwa jina la Ashraf, alimwambia kuwa lazima wawasiliane na ndugu wengine kwa hatua hiyo.

Pamoja na wazo hilo kukubalika, Nyerere alibaki pembeni na hata alipoulizwa zaidi kuhusu utaratibu alikataa kwa kuwa si mwanakamati wa kamati ya maziko

“Mimi sihusiki na chochote kwani nimekuwa nikitukanwa kwamba nakusanya fedha za rambirambi kisha nazitafuna,” anasema.

No comments:

Post a Comment