Haji Manara: Nitaachia Ngazi Ndani ya Simba Endapo Timu Itapoteza Dhidi ya Arusha United Leo - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 15 August 2018

Haji Manara: Nitaachia Ngazi Ndani ya Simba Endapo Timu Itapoteza Dhidi ya Arusha United Leo

Ofisa Habari wa Simba SC, Haji Manara, amesema ataachia ngazi ndani ya klabu hiyo endapo timu yake itapoteza mchezo dhidi ya Arusha United leo.

Manara ametoa kauli hiyo kuelekea mchezo wa leo wa kirafiki ambapo Simba itacheza na Arusha United kufuatia mwaliko maalum na Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo.

Ofisa huyo amefunguka akiamini kuwa Simba haiwezi kufungwa na Arusha United huku akitamba kumuahidi kipigo Gambo katika kipute hicho.

"Kama Arusha United wakishinda leo mimi nitaachia rasmi ngazi ndani ya Simba, siamini kama wanaweza wakatufunga" alisema.

Aidha, uongozi wa Simba umesema utautumia mchezo huo kama sehemu ya kuiandaa na mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugar.

Simba watakapiga na Mtibwa jijini Mwanza Agosti 18 ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba ukiwa unaahsiria kufunguliwa rasmi kwa pazia la Ligi Kuu Agosti 22 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment