Haji Manara Ampongeza Canavaro Baada ya Kustaafu Soka Awapa Ushauri Huu Yanga - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 13 August 2018

Haji Manara Ampongeza Canavaro Baada ya Kustaafu Soka Awapa Ushauri Huu Yanga

Baada ya aliyekuwa beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro. kutangaza kustaafu soka, Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amefunguka na kumpa heshima yake mkongwe huyo.

Manara ameeleza kuwa Cannavaro ni moja ya mabeki bora kuwahi kutokea katika taifa hili la Tanzania ndani ya miaka 10 iliyopita.

Manara ameshauri itakuwa vema kama Cannavaro akaagwa kwa mechi moja kupigwa Uwanja wa Taifa baina ya timu yake 'Friends Of Nadir' dhidi ya Yanga kutokana na mchango wake ndani ya soka la Tanzania.

Lakini licha ya kushauri hilo, Cannavaro aliagwa jana kwenye wa Jamhuri Morogoro kwa Yanga kukipiga na Mawenzi Merket ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Baada ya kustaafu, Cannavaro alikabidhi jezi yake yenye namba 23 kwa beki Abdallah Shaibu 'Ninja' ambaye atakuwa anaivaa kwa mechi zijazo akiwa na kikosi hicho.

No comments:

Post a Comment