H. Baba amfungukia Rich Mavoko, adai WCB sio wanyonyaji - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 15 August 2018

H. Baba amfungukia Rich Mavoko, adai WCB sio wanyonyajiMsanii wa Bongo Fleva, H. Baba ametoa mtazamo wake kwa kile kinachoendelea kati ya Rich Mavoko na WCB.


Muimbaji huyo ameeleza kuwa WCB hawawezi kumnyonya msanii, hivyo tofauti iliyopo kati ya WCB na Rich Mavoko ni vyema wakakaa chini na kusuluhisha. 


==>Kupitia Instagram ameandika;

"Diamond Platnumz Pole sana ni muda wa kujifunza maisha na watu ni vitu viwili tofauti, umakini ulionao wewe sio wa kila binadamu anaumakini huo kujitambua kwako nakujipambania kwa uwezo wako na kumuomba Mungu sio Jambo la kawaida kwa mdharau Mwiba.


Kama kuna tofauti yako na Mr. Mavoko limalizeni kiustaarabu naamini mnafahamiana vyema toka kitambo. Mimi natoka mwanza nimewakuta kwenye game japokuwa siku ya kila mmoja kutoboa Mwenyezi Mungu ameiwekea siri kubwa ili usikate tamaa.


Amkukata tamaa Kila mmoja akatoboa kwa njia yake Onyeshaneni upendo Sanaa inasiri kubwa kioo cha jamii kwa msanii ni ishu kubwa Sana ila tunachukulia poa jambo hili. Wekeni sawa swala lenu #Unyonyaji unaosemekana kuwa #WCB ni wanyonyaji sio kweli.


WCB hawana uwezo wa kumnyonya msanii ila msanii ana uwezo wakuwanyonya WCB kwa sababu nyingi sana watazame kina MBOSO LAVA LAVA je ni nani ana mnyonya mwenzie, utagundua WCB wana utu, niwapambanaji ila kama upambani auwendani na kasi ya Diamondn lazima utaomba poooo.


Uvumilivu kwenye Sanaa ndio misingi ya sanaa yetu, ukifuata ya walimwengu utakuwa mtazamaji wa walimwengu. Nina mengi ya kusema kwa Leo niishie hapa #lawama sio mzigo..."


Hapo jana August 14, 2018 Diamond na uongozi wa WCB walifika Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kufuatilia suala hilo mara baada ta Rich Mavoko kufika hapo awali ambapo inaeleza alipoleka mkataba kati yake na lebo hiyo ambao anadai ulikuwa wa kinyonyaji.

No comments:

Post a Comment