Gigy Money Atamani Mtoto wake Awe na Tabia Kama zake - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 15 August 2018

Gigy Money Atamani Mtoto wake Awe na Tabia Kama zakeMsanii wa bongo fleva na 'video vixen' nchini, Gigy Money amesema atajisikia furaha na amani endapo mtoto wake wakike aliyempa jina la Mayra, kuja kuishi kama alivyokuwa yeye kwa madai 'role model' wa mtoto ni mama pekee nasio mtu baki. 

Gigy ametoa kauli hiyo leo Agosti 14, 2018 wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, na kusema haiwezi ikatokea mtoto akawa na role model tofauti na mtu ambaye amemzaa. 

"Kila mtoto yoyote 'role model' wake ni mama yake mzazi hata iwaje.  Uwezi kusema mwanao atakuwa 'role model' wa mtu mwingine. Hivyo mwanangu atakuwa tu vyovyote atakavyotaka kuwa mimi nitampa ushirikiano. siwezi kumlaumu hata akitaka kuwa kama mimi ila ndio ntazidi kufurahi", amesema Gigy. 

Pamoja na hayo, Gigy ameendelea kwa kusema "siwezi kujutia kuzaa halafu kingine ni kwamba kujipanga utajipanga baada huko wala hupaswi kuwaza kuwa itakuaje nikifanya jambo fulani. Maisha ya siku hizi hayana hiyo kitu, Mungu yupo kila siku anatenda". 

Hii si mara ya kwanza kwa msanii Gigy Money kutoa kauli kama hizo kwani hata Juni 27, 2018 alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI alitoa kali ya mwaka kuwa hakumbuki idadi ya mimba alizowahi kutoa licha ya kudai jambo hilo sio ufahari, huku akisisitiza zaidi kuwa ana lengo la kuanzisha timu ya mpira kupita watoto wake.

No comments:

Post a Comment