FEI TOTO ASHANGAZWA NA MKONGOMANI YANGA - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 8 August 2018

FEI TOTO ASHANGAZWA NA MKONGOMANI YANGA


Kiungo mpya wa Yanga, Feisal Abdallah Salum ‘Fei Toto’ ameonekana kush­angazwa na namna ambavyo kocha wa kikosi hicho, Mwinyi Zahera anavyowanoa.

Fei Toto aliyejiunga na Yanga hivi kar­ibuni akitokea JKU ya Zanzibar, amesema Zahera amekuwa na vitu vingi anapow­afundisha jambo ambalo litamfanya kiwango chake kikue zaidi.

Kwa mujibu wa Championi, Fei Toto alisema Zahera ni msaada mkubwa kwake, hivyo anaamini atafanya makubwa zaidi akiwa na Yanga.

“Zahera ni kocha mzuri na mazoezi ambayo anatupa ni mazuri kwani ana vitu vingi ambavyo hutupa­tia, naamini nikiwa hapa nitakua zaidi na nitafika mbali kisoka,” alisema Fei Toto.

Yanga kwa sasa ipo kam­bini mkoani Morogoro ikijiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tan­zania Bara unaotarajiwa kuanzia Ago­sti 22

No comments:

Post a Comment