DIAMOND, MAVOKO WAMALIZA TOFAUTI ZAO - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 15 August 2018

DIAMOND, MAVOKO WAMALIZA TOFAUTI ZAO


Mkurugenzi wa Kampuni ya WCB, ambaye pia ni staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul  ‘Diaomond Platnumz’ na Mameneja wake wawili, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ na Sallam Sharraf wametinga katika ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kuitikia wito wa baraza hilo kuhusu malalamiko yaliyowasilishwa na mwanamuziki Rich Mavoko aliyedai kuwa mkataba wake na WCB ni wa kinyonyaji.

Akizungumzia hilo mmoja wa meneja wa Diamond, Sallam, amesema waliitwa na Basata na sasa wapo katika mazungumzo ya kutatua jambo hilo na kufikia mwafaka.

Sallam amesema ni vyema watu wakasubiria yatakayoamuliwa huko, ambapo wanaamini Basata itauambia umma nini kilichoafikiwa badala ya wao  kuwa wasemaji.

No comments:

Post a Comment