DE GEA AJIANDAA KUWAZIDI NOTI MAKIPA WOTE DUNIANI - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 15 August 2018

DE GEA AJIANDAA KUWAZIDI NOTI MAKIPA WOTE DUNIANI


Baada ya kushindwa kujiunga na Real Madrid, kipa wa Manchester United, David de Gea anajiandaa kuwa kipa ghali zaidi duniani.

De Gea alikuwa anatakiwa na Madrid kwa muda mrefu lakini akashindwa kujiunga na timu hiyo na sasa anajiandaa kusaini mkataba mpya na United.

Kipa huyo anatarajiwa kusaini mkataba wa pauni 200,000 kwa wiki ambao ni zaidi ya shilingi milioni 500, ambapo atakuwa ndiye analipwa ghali zaidi kwa makipa kwenye Ligi Kuu England.

Mbali na kuwa kipa ghali, De Gea pia anatajwa kuwa kipa mahiri zaidi duniani kwa sasa.

Hata hivyo, inaonekana pia kuwa kipa huyo tayari ameshaweka kambi United kwa kuwa timu pekee iliyokuwa inamwania ni Madrid ambayo imeshamchukua kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois.

No comments:

Post a Comment