DC Jokate Mwegelo Akubali Ombi la Mwanafunzi Darasa la 7 Aliyemwandikia Barua - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 11 August 2018

DC Jokate Mwegelo Akubali Ombi la Mwanafunzi Darasa la 7 Aliyemwandikia BaruaMkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, amekubali ombi la mwanafunzi Mwanahamisi Yusufu wa darasa la Saba wa Shule ya msingi ya Chanzige B, Kisarawe ya kumtaka aitembelee shule yao.


Jokate ameandika katika ukurasa wake wa Instagram  leo Agosti 11 na kusema kuwa mwanafunzi huyo alimuandikia barua na akaipokea Jumanne, Agosti 7.


==>Huu ni Ujumbe wa DC Jokate Mwegelo.

"Siku ya Jumanne, tarehe 07/08/2018 nlipokea barua ya Mwanahamisi Yusufu Sakidukuli, mwanafunzi wa darasa la 7 - iliyodhaminiwa na Mwalimu Mkuu wake, kutoka shule ya msingi Chanzige B hapa Kisarawe. 

"Aliniomba nitembelee shule yake niongee na wanafunzi wenzake wa darasa la 7, kwa ajili ya mazungumzo juu ya changamoto mbali mbali shuleni hapo na elimu kwa ujumla hapa Kisarawe.

"Jana tarehe 10/08/2018 nikifuatana na Afisa Elimu- Msingi Wilaya na Katibu Tawala Wilaya tulifanikiwa kufika shule ya Msingi Chanzige, pamoja na matembezi katika mazingira ya shule, nilifanya vikao na Mwanahamisi, Wanafunzi wa darasa la 7 na Walimu. Tulijadili changamoto za Afya, Elimu na Miundo Mbinu. Nilifurahi jinsi Mwanahamisi alivyoweza kujipambanua na uthubutu alioonyesha. .

"Bado changamoto za masuala ya hedhi salama kwa Vijana Balehe ni kubwa, miundo mbinu ya elimu bado changamoto hususani makazi ya waalimu. 

"Changamoto ya maji tayari imetafutiwa suluhu kuna mradi unaendelea wa kuleta maji kutoka Ruvu Juu kuja Kisarawe wenye thamani ya Tsh Bilioni 10.8.

"Mimi, pamoja na Mwanahamisi, kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa masuala ya elimu, afya, mazingira na huduma nyingine za kijamii tumedhamiria kuleta mabadiliko kwenye changamoto hizi, ili kuhakikisha juhudi za Rais John Joseph Pombe Magufuli katika kuleta Elimu Bora, Afya Bora na Mazingira Salama ya kielimu Wilayani Kisarawe zinakua halisi.

"Nimshukuru Mwanahamisi, Wanafunzi na Uongozi wa shule ya Chanzige A na B kwa kushirikiana nami kujadili na kunia pamoja kuleta mabadiliko haya.

"Mwanahamisi ni mfano mzuri wa viongozi tunaowatengeneza leo kwa ajili ya kulijenga taifa letu. Lakini hasa ni mfano mzuri wa jinsi jamii inatakiwa kushiriki katika maendeleo yake na kutatua changamoto pamoja na serikali yake. .

"Niendelee kuwakaribisha Wilaya ya Kisarawe wadau mbali mbali wa masuala ya Afya ya Uzazi kwa Vijana Balehe, Wadau wa Elimu na Miundo Mbinu, pamoja tujadili na kuamua namna gani Serikali ya Awamu ya Tano inaweza shirikiana nanyi hapa Wilaya ya Kisarawe kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya Elimu."

No comments:

Post a Comment