COASTAL UNION KUSAINI MKATABA NA MDHAMINI MPYA LEO - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 15 August 2018

COASTAL UNION KUSAINI MKATABA NA MDHAMINI MPYA LEO


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Coastal Union unasaini mkataba na mdhamini mpya leo kwa ajili ya kutia nguvu katika kikosi cha timu hiyo.

Taarifa za uhakika kutoka Tanga zinasema klabu hiyo imefikia mwafaka na Msanii Ali Kiba kuingia naye mkataba wa udhamini kupitia kinywaji chake cha Mofaya.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Kiba kuingia mkataba wa mwaka mmoja na Kiba kwa ajili ya kuichezea Coastal Union ambaye imerejea Ligi Kuu Bara.

Mkataba wa Kiba na Coastal hautambana kufanya kazi zake za muziki hivyo atakuwa huru kuendelea na majukumu yake nje ya mpira pale inapobidi.

Kikosi hicho kipo katika maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi ambao pazia lake litafunguliwa Agosti 22 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment