Buriani:Safari ya Mwisho ya Mzee Majuto Yakamilika Azikwa Tanga - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 10 August 2018

Buriani:Safari ya Mwisho ya Mzee Majuto Yakamilika Azikwa Tanga

Mwili wa muigizaji wa vichekesho Amri Athumani maarufu kama Mzee King Majuto utazikwa leo nyumbani kwake Donge, Tanga nchini Tanzania.

Mwili wake ulisafirishwa jana usiku hadi Tanga ambapo ulisimamishwa njiani kuwapa mashabiki fursaya kutoa heshima zao za mwisho.

Dua ya kuaga mwili wa marehemu huyo aliyefariki Jumatano usiku akitibiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ilifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam

Miongoni mwa waliohudhuria ni Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli.

Watanzania walivyomuomboleza King Majuto
Leo ibada ya mazishi inatarajiwa kuanza mwendo wa saa sita mchana katika msikiti wa Nuruguda uliopo karibu na nyumbani kwake.

Baadaye mwili wake utazikwa kijiji cha Kiruku yalipo mashamba yake nje kidogo ya jiji la Tanga.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la Tanzania, mwili ulipowasili nyumbani kwa Mzee Majuto mwendo wa saa moja unusu usiku, kuliibuka vilio huku wanawake wengi wakizimia.

Mwili ulisimamishwa katika vijiji 14 na mashabiki wakitaka kutoa heshima ya mwisho.

No comments:

Post a Comment