Breaking: Rais Magufuli Amefanya Uteuzi Mpya wa Viongozi - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 13 August 2018

Breaking: Rais Magufuli Amefanya Uteuzi Mpya wa Viongozi

RAIS John Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uteuzi wa  wakuu wa wilaya kufuatia aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Chato, Kanali Patrick Songea,  kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi nje ya nchi.Akisoma uteuzi huo, Katibu Mkuu, Balozi Mhandisi, John Kijazi, rais amemhamisha kituo Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Mtemi  Simeon kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato.

Pia amemteua Bi. Senyi Mganga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba. Uteuzi huo unaanza leo na wateule hao wanatakiwa kuripoti kazini mara moja.Mbali na uteuzi huo, amewateua wakurugenzi wapya wa wilaya, manispaa, miji na majiji na na wakurugwenzi 41 na kuwahamisha wengine 19.

No comments:

Post a Comment