Breaking News: Muigizaji mkongwe Mzee Majuto afariki dunia - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 8 August 2018

Breaking News: Muigizaji mkongwe Mzee Majuto afariki dunia

Msanii mkongwe wa vichekesho Amri Athuman’ King Majuto’ amefariki dunia usiku huu baada ya kulazwa siku chache zilizopita katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Mchekeshaji Joti ndio wa kwanza kutoa taarifa hizo kupitia mtandao wa instagram.
“R.I.P @Kingmajuto Umetuachia Maumivu Makubwa sana ktk Tasnia ya Comedy Tanzania Sisi wanao,Tutakukumbuka kwa kazi zako,Upendo wako,Tabasamu lako Daima milele,Tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi,Pumzika kwa Amani Mzee wetu,” aliandika Joti.
Mzee Majuto ambaye alijizolea umaarufu mkubwa kwenye filamu alianza kuugua mwaka jana na mwaka huu serikali kwa kushirikana na wananchi walichanga pesa na kumpelekeka kwenye matibabu nchini India.
Muigizaji huyo alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9.

No comments:

Post a Comment