BREAKING NEWS: MKWASA AFANYIWA UPASUAJI WA MOYO, SASA YUKO ICU INDIA - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 5 August 2018

BREAKING NEWS: MKWASA AFANYIWA UPASUAJI WA MOYO, SASA YUKO ICU INDIA


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa amefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo.

Mkwasa yuko jijini New delhi, India ambako amefanyiwa upasuaji huo mkubwa na imeelezwa bado yuko katika chumba cha usimamizi maalum, yaani ICU.

“Kweli Mkwasa amefanyiwa upasuaji wa moyo nchini India. Alikwenda kule akiambatana na mkewe Betty Mkwasa,” alisema mmoja wa ndugu wa familia ya Mkwasa.

Awali, wakati akielezwa alitaka kujiuzulu Yanga, Mkwasa alisema hali yake kiafya haikuwa nzuri. Wengi waliona kama alitaka kukimbia matatizo kwa kuwa klabu hiyo ilikuwa ikiandamwa na ukata.

No comments:

Post a Comment