Bonge la Nyau Afunguka Sababu za Kutoka na Khadija Kopa - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 11 August 2018

Bonge la Nyau Afunguka Sababu za Kutoka na Khadija KopaMsanii wa hip hop, Lameck Philipo maarufu kama 'Bonge la Nyau' ametoa sababu ya kufanya mziki na mkongwe wa muziki wa Taarab na anaeendelea kufanya vizuri, Khadija Kopa ambapo amesema lengo ni kuleta ladha tofauti na ile iliyozoeleka.

Bonge la nyau amefunguka kuwa ngoma hiyo inayotarajiwa kutoka hivi karibuni itawakutanisha mashabiki wa mziki wake na mashabiki wa Taarab na kuweza kufurahia kwa pamoja muunganiko huo. Akiongea na Mikito Nusunusu Nyauloso amesema 

“Watu wanaweza kufikiri nimefanya Taarab pia kwenye kolabo yangu na Khadija Kopa, lakini si hivyo, tumefanya kitu tofauti na kitaleta matokeo tofauti kwenye gemu ambayo yatawashangaza wengi,” .

No comments:

Post a Comment