Billnass Akanusha Kuwa Chanzo cha Steve Kususia Msiba wa Mzee Majuto - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 10 August 2018

Billnass Akanusha Kuwa Chanzo cha Steve Kususia Msiba wa Mzee MajutoMsanii wa bongo fleva Billnass amekanusha taarifa kuwa yeye ndio chanzo kikubwa cha kumkwaza msanii wa bongo movies Steve nyerere kujihusisha na shughuli za msiba wa Mzee Majuto na misiba mingine itakayofuata kutokana na kashfa za kuwa anahujumu pesa za ubani zinazopatikana katika misiba.

Billnass na Stev Nyerere waliwahi kuingia katika majibizano yaliyopelekea wawili hao kuonekana kushushiana heshima hasa baadaya billnass kusema kuwa steve amekiwa akisubiri misiba ili apate ulaji, hata hivyo mara baada ya kutokea kifo cha mzee majuto billnass aliandika maoni katika moja ya post iliyozunguka sana katika mtandao ikisema kuwa kipindi hiki cha msiba wa mzee ndio kipindi cha Steve kukusanya pesa za ada ya watoto.


Hata baada ya maneno mengi, Steve Nyerere alisema kuwa kwa sasa yeye atakuwa kama waombelezaji wnegine lakini hawezi kujihusisha na kitu chochote katika misiba.

Billnass afunguka “sio kweli , mimi sio chanzo cha steve kususia msiba wa mzee,kwani mbona hata mimi aliniambia kuwa nina wafuasi kumi lakini sikuacha muziki.na atambue kuwa ni maneno tu kwaio asife moyo aendelee kujitolea.”

Hata hivyo maneno hayo ya kumkashifu msanii Steve Nyerere yaliwagusa wasaniiwengi na kuamua kuliongelea hilo huku wakionekana kutopendezwa na tuhuma hizo zinazoendelea juuu ya msanii mwenzao.

No comments:

Post a Comment