BASATA WATOA MAAMUZI JUU YA SAKATA LA DIAMOND NA MAVOKO - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 15 August 2018

BASATA WATOA MAAMUZI JUU YA SAKATA LA DIAMOND NA MAVOKO


Kufutia sakata linayoendelea kati ya Mwanamuziki Rich Mavoko na Lebo ya WCB inayoongozwa na Diamond Platnumz, suala hilo limetua mikononi mwa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) na kupokea malalamiko ya Mavoko kuhusiana na mkataba wake na lebo hiyo ambao alidai ni wa kinyonyaji.

Baada ya kupokea malalamiko hayo, Basata imemuita Diamond na viongozi wake ambao ni Mkubwa Fella, Sallam na Babu Tale, leo Agosti 14, 2018 na kuzungumza nao katika ofisi za Basata zilizopo jijini Dar es Salaam.

Uamuzi uliotolewa na walezi hao wa sanaa nchini ni kuandaa kikao kitakachokutanisha pande zote mbili yaani Diamond na Mavoko kisha wayazungumze na kufikia muafaka.

No comments:

Post a Comment