Babu Tale Afunguka Kuhusu 'In love and Money Tour’ ya Vanessa na Jux ''Imetupa Changamoto Wasafi Festival'' - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 6 August 2018

Babu Tale Afunguka Kuhusu 'In love and Money Tour’ ya Vanessa na Jux ''Imetupa Changamoto Wasafi Festival''

Mmoja kati ya waratibu wa Wasafi Festival, Babu Tale amedai walichokifanya wapenzi wawili, Jux na Vanessa kupitia tamasha lao la In love and Money Tour ni changamoto kwa tamasha lao ambalo linatarajiwa kuzunguka katika mikoa 12 siku za usoni.

Tamasha la In love and Money Tour limeweza kuzunguka katika mikoa mitano, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mtwara pamoja na Dar es salaam na kuonyesha mafanikio makubwa sana kwani mashabiki wengi waliweza kujitokeza na kufanikiwa kujaza viwanja mbalimbali.

Tale aliiambia Bongo5 kwamba mafanikio makubwa na tamasha hilo ni changamoto kwa tamasha la Wasafi Festival ambayo litaanza kutimua vumbi miezi michache ijayo.

“Hii ni ishara ya muziki unakuwa, nchi zilizoendelea kila mwisho wa wiki unajua kuna show kubwa, kwahiyo hii ni ishara nzuri ukiangalia Vanessa amejaza viwanja kibao. Mimi nikiwa kama kiongozi au mratibu wa Wasafi Festival inanipa changamoto naanza mkoa gani? sisi tunafanya show zaidi ya mikoa 12 na tunapiga na Dar es salaam inakuwa histori,” alisema Babu Tale.

Aliongeza “Uzuri Diamond na familia yake ya Belaire inakuja kumsupport, ni kitu kikubwa sana,”

Show hiyo inasubiriwa kwa hamu ya mashabiki wa muziki nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment