Baada ya Kuwagalagaza WCB Rich Mavoko Awashukuru Basata "Mama ni Mama Hata Kama Kilema" - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 10 August 2018

Baada ya Kuwagalagaza WCB Rich Mavoko Awashukuru Basata "Mama ni Mama Hata Kama Kilema"

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Rich Mavoko amejitokeza kwa mara ya kwanza kuelezea sakata la kukutana na BASATA kuwasilisha mkataba wake aliosaini na WCB aliodai kuwa unamkandamiza.

Mavoko kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa anashukuru kukutana na BASATA na kupata elimu ya kutosha huku akiwamwagia sifa kuwa hao ndio maana halisi ya walezi wa sanaa yetu nchini Tanzania.

"Nimejifunza vingi ila la muhim  kabisa  nimeona Umuhim wa kukaa karibu na  walezi wetu mana changamoto ni nyingi na  kuna mengi ila yote mnaweza yajua kama tukiwa karibu nanyi leo mmenipa maana ya neno mama ni mama ata kama ni kilema, ata iweje nyinyi ndo walezi wasanaa Yetu Niseme Tu Asante"


Leo Alhamisi Agosti 9, 2018 Rich Mavoko amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza ambapo amepeleka mkataba wake na WCB akidai uangaliwe upya kwani umekuwa ni wa unyonyaji.

No comments:

Post a Comment