BAADA YA KUMCHANA KLOPP, RAMOS SASA AHAMIA KWA RONALDO - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 16 August 2018

BAADA YA KUMCHANA KLOPP, RAMOS SASA AHAMIA KWA RONALDO


Kitendo cha Cristiano Ronaldo kuondoka Real Madrid kuelekea Italia katika klabu ya Juventus, kimemuibua kivingine beki katili, Sergio Ramos.

Nahodha huyo wa Madrid ameibuka na kusema kuwa kuondoka kwa Ronaldo hakuwezi kuizua Real Madrid kuchukua mataji kutokana na ukubwa wake.

Ramos amesema uamuzi wa Ronaldo kuondoka hautaweza kuipunguzia chochote Madrid ambayo imekuwa na historia kubwa kimpira na ikiwa na mataji mengi makubwa.

Beki huyo ameamua kufunguka baada ya wadau wengi wa soka kusema Madrid kwa sasa itayumba baada ya nyota huyo kuikacha timu hiyo kutokana na mchango wake haswa katika safu ya ushambuliaji.

No comments:

Post a Comment