Aua mke kwa Shoka Kisha Kujinyonga Kisa Wivu wa Mapenzi - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 2 August 2018

Aua mke kwa Shoka Kisha Kujinyonga Kisa Wivu wa Mapenzi

MWANAMKE mkazi Njage wilayani Kilombero Mkoa wa Morogoro, ameuawa kwa kukatwa kwa shoka kichwani na mumewe kwa kilichoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Willibrod Mutafungwa, alisema hayo jana na kufafanua kuwa tukio hilo lilitokea Julai 28 majira ya asubuhi ambapo mwanamke huyo, Rose Mngwe (43),  aliuawa na mumewe, Jacob Kambo (45), mkazi wa Kijiji cha Njage.

Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, mwanaume huyo baada ya kumuua mkewe kwa kumkata kwa shoka kichwani, alikimbilia porini na kujinyonga kwenye mti kwa kutumia kamba.

Kamanda Mutafungwa alisema inadaiwa kuwa mwanaume huyo aliamua kufanya kitendo hicho baada ya kuona mkewe amempuuza alipomwambia kuwaondoa watoto wake wa kike aliowazaa nje ya ndoa.

Kamanda alifafanua kuwa alitaka waende kwa waliomzalisha  watoto hao kwa madai kuwa wanawanyima nafasi wakiwa hapo.

Alisema miili ya marehemu hao imeshakabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya kuendelea na shughuli za mazishi.

Katika tukio lingine, Leo Charles Mashaka (61), mkazi wa Kitongoji cha Igagafu wilayani Kilosa, ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye butu kichwani na usoni na mtoto wake wa kumzaa, Emmanuel Leo Charles, sababu ikitajwa ni kudai urithi.

Kamanda Mutafungwa alisema tukio hilo lilitokea Julai 30, alfajiri katika Kata ya Lumuma Tarafa ya Idete ambapo Mashaka alimpigwa na kitu chenye butu kichwani na usoni upande wa kulia na kumsababishia jeraha na michubuko mgongoni, Alisema tukio hilo lilisababishwa na mgogoro katika familia kuhusu urithi.

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa alikamatwa na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

No comments:

Post a Comment