Askari wa JWTZ Auwawa kwa Kupigwa Risasi - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 11 August 2018

Askari wa JWTZ Auwawa kwa Kupigwa Risasi

Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kutoka Burundi wamemuua kwa kumpiga risasi Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania aliyekuwa akishirikiana na wananchi kuwasaka majambazi walioteka gari la abiria.

Gari hiyo yenye namba za usajili T 757 AWG  Toyota Hiace ilikuwa ikitokea Mjini Kasulu kwenda Kijiji cha Nyamugari Wilayani Buhigwe na majambazo hao kupora vitu mbalimbali.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji saba vya Tarafa ya Muyama, baada ya kufanya msako, Mkuu wa wilaya ya Buhigwe, Luteni-Kanali MARKO NGAYALINA amepiga marufuku tabia ya baadhi ya wananchi kuwahifadhi raia wa Burundi kinyume cha sheria.

Luteni - Kanali NGAYALINA amesema wengi wa raia hao wa Burundi wamekuwa wakifanya vitendo vya uhalifu na kuondoka kutokana na wilaya hiyo kuwa mpakani.

Baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo wamesema wamechoshwa na kuwepo kwa matukio ya mara kwa mara ya uvamizi unaofanywa katika maeneo yao.

No comments:

Post a Comment