Alikiba Achafua Hali ya Hewa... Awaweka Mashabiki Zake Njia Panda - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 15 August 2018

Alikiba Achafua Hali ya Hewa... Awaweka Mashabiki Zake Njia Panda

Msanii wa BongoFleva mwenye 'hit song' ya 'Mvumo wa Radi', Alikiba amewaacha njia panda mashabiki zake baada ya yeye kuweka picha mfululizo kwa siku moja katika mtandao wake wa Instagram, jambo ambalo limewafanya kufikiri kuwa ni ujio wake mpya wa kutoa wimbo baada ya kukaa kimya kirefu.

Muda mchache kupita baada ya kuwekwa picha hizo, mashabiki hao walimiminika katika na kuanza kutoa maoni yao binafsi mbalimbali, huku wengine wakijaribu kumshauri kwa namna moja ama nyingine juu ya sanaa yake.

Miongoni mwa ujumbe zilizokuwa zikitawala chini ya picha hizo ni pamoja na;

"Naziona dalili zote za wimbo mpya yakufungia mwaka", ameandika barrish_holictz.

"The king always is different with other people kimawazo kifikra pia hata kwenye kufanya mambo yake. Huwa halazimishi kabisa kufanana na wengine 'like that guy'. Yani ni mtu makini sana na hana ushindani kwenye 'game' maana anaamini kipaji chake, wanao toa nyimbo 100 na yeye wimbo moja halafu wewe uliotoa moja inakua homa ya jiji kuliko waliotoa nyimbo 100", ameandika chii_beiby_quetface.

"Kwa mapicha picha haya bila shaka 'new hit is coming", ameandika prince_blessed

"Achia dude mzee baba", ameandika officialgerard_hero

"Nasikia harufu ya ngoma mpya", ameandika officia_topdenny251Hii si mara ya kwanza kwa Alikiba kutumia njia ya aina hiyo kuweka 'attention' kwa watu kwani itakumbukwa mnamo mwezi Agosti mwaka 2017, alifanya vitu kama hivyo alipokuwa kwenye show yake mjini New York nchini Marekani na baada ya kupita siku kadhaa alitoa wimbo wake wa 'Seduce Me' ambao hadi sasa umetazamwa na takribani watu milioni 9.94 kupitia akaunti yake ya 'Youtube'.

Kwa upande mwingine, Alikiba siku ya Ijumaa anatarajia kufanya show katika mji wa Toronto nchini Canada ambapo atakuwa na wasanii wengine kama Yemi Alade, Falz the Bahd Guy, Sheebah, Dj Spinall, Zahara, Nonso Amadi pamoja na Nsoki.

No comments:

Post a Comment