ALI KIBA AIDHAMINI COASTAL UNION NA KINYWAJI CHAKE 'MOFAYA' - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 14 August 2018

ALI KIBA AIDHAMINI COASTAL UNION NA KINYWAJI CHAKE 'MOFAYA'


Imeelezwa kuwa Msanii Ali Saleh Kiba ambaye ameingia mkataba wa mmoja kuichezea Coastal Union ya Tanga, ameidhamini klabu hiyo kupitia kinywaji chake cha Mofaya.

Mbali na kusaini mkataba wa mwaka mmoja, Kiba amefikia makubaliano na uongozi wa Coastal Union ambapo sasa atakuwa anakitangaza kinywaji chake.

Kinywaji cha Mofaya bado hakijaingia sokoni hapa nchini kutokana na Balozi wake, Ommy Dimpoz kupatwa na matatizo ya kiafya.

Kiba ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kupitia sanaa yake ya muziki, atakuwa anakitumikia kikosi cha Coastal Union ya Tanga japo mkataba wake unamruhusu kufanya kazi zake zake za muziki.

Mkataba huo haujambana Kiba kutokana na muziki kumfikisha hapo alipo, hivyo atakuwa anacheza mpira pale ambapo nafasi itakapokuwa inaruhusu kwake.

No comments:

Post a Comment