Zlatan aifanya kitu mbaya klabu ya Orlando City Marekani (+Picha - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 30 July 2018

Zlatan aifanya kitu mbaya klabu ya Orlando City Marekani (+Picha

Mshambuliaji wa klabu ya Los Angeles Galaxy, Zlatan Ibrahimovic ameendeleza utawala wake wa kupachika mabao nchini Marekani baada ya kuifungia ‘hat-trick’ timu yake dhidi ya Orlando City.
Kwenye ushindi wa jumla ya mabao 4 – 3 uliyopata LA Galaxy dhidi ya Orlando City nyota huyo wazamani wa timu ya taifa ya Sweden aliweza kufikisha jumla ya magoli 15 kwenye michezo yake 17 aliyocheza kwenye ligi ya Marekani (Major League Soccer).
Kwa matokeo hayo yanaifanya timu hiyo ya  LA Galaxy kucheza michezo tisa pasipo kufungwa nakuifanya kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ya MLS.
Hii inakuwa ‘hat-trick’ yake ya kwanza Ibrahimovic tangu alivyofanya hivyo alipoifungia Manchester United mabao matatu ilipoikabili timu ya Saint-Etienne Februari 26 kwenye michuano ya UEFA Europa League.

No comments:

Post a Comment