Zimbabwe wanafanya uchaguzi mkuu leo, Mzee Mugabe akisaliti chama chake cha ZANU-PF - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 30 July 2018

Zimbabwe wanafanya uchaguzi mkuu leo, Mzee Mugabe akisaliti chama chake cha ZANU-PF

Wananchi nchini Zimbabwe leo Julai 30, 2018 wanafanya uchaguzi mkuu wa urais, serikali za mitaa na wabunge.

Rais Mnangagwa akiwa na Robert Mugabe
Uchaguzi huo unakuwa wa kwanza katika historia ya Taifa hilo kufanyika bila kuwepo kwa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe.
Wagombea wakuu wenye nguvu katika uchaguzi huo wa urais ni Rais wa Sasa Emmerson Mnangagwa wa chama tawala cha Zanu-PF na kiongozi wa upinzani Nelson Chamisa.
Chamisa (40) ambaye anakiwakilisha Chama Cha Movement For Democratic Change (MDC) ameonekana kuwashawishi watu wengi hususani vijana nchini humo.
Kwa upande mwingine, Mzee Robert Mugabe jana Jumapili Julai 29, 2018 akizungumza na waandishi wa habari nyumbani amewashangaza watu wengi hususani wanachama wa Chama Cha ZANU-PF baada ya kusema kuwa atampigia kura kiongozi wa upinzani.
Akifunga Kampeni hapo jana Rais Mnangagwa (75) almaarufu kwa jina la MAMBA ameahidi kufanya mageuzi ya kiuchumi ikiwemo kutoa ajira kwa vijana.
Naye, Chamisa akiahidi kuijenga upya Zimbabwe ambapo alisikika akitilia mkazo wa kulibadilisha jina la Zimbabwe Kama alivyoahidi kwenye Kampeni zake zote alizofanya akidai jina la sasa lina laana.
Tayari mamia ya waangalizi wa uchaguzi wametumwa kuhakikisha uchaguzi huo wa kihistoria unakwenda sawia

No comments:

Post a Comment