YANGA WATAJA SABABU ZA KUMKATAA MZIMBAMBWE WA SINGIDA UNITED - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 27 July 2018

YANGA WATAJA SABABU ZA KUMKATAA MZIMBAMBWE WA SINGIDA UNITED


Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, umefunguka na kueleza sababu za kumkataa beki Elisha Muroiwa waliyepewa na Singida United.

Nyika amesema Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema hana mpango na beki huyo Mzimbambwe kutokana wachezaji walionao kujitosheleza.

Aidha, kwa mujibu wa Nyika, Zahera amesema Muroiwa asingeweza kupata nafasi Yanga sababu hakuwa kwenye mapendekezo yake hivyo akaona ni vema akarejea kuendelea na mkataba na klabu ya Singida.

"Unajua timu inaposajili mchezaji inakuwa ina lengo naye kuwa namna ipi atumike, sasa klabu kama Yanga ni kubwa, haiwezi ikatokea tu inaletewa mchezaji ambaye hakuwa katika mipango ya mwalimu" alisema Nyika.

Singida United kupitia kwa Mlezi wake, Mwigulu Nchemba, iliamua kuwasaidia Yanga mchezaji huyo kutokana na kuwa katika kipindi cha mpito ili aweze kuwa sehemu ya kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria japo mwisho wa siku msaada huo umegonga mwamba.

No comments:

Post a Comment