Wimbo mpya wa ‘Happy’ wa Rich Mavoko waibua mapya, mashabiki wake wampongeza kuondoka WCB - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 23 July 2018

Wimbo mpya wa ‘Happy’ wa Rich Mavoko waibua mapya, mashabiki wake wampongeza kuondoka WCB

Tangu msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rich Mavoko aachie ngoma yake mpya ya ‘Happy’ kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii maoni mengi ya mashabiki wake yamekuwa yakiongozeka kila siku wengi wakimpongeza.

Maoni hayo licha tu ya kumpongeza kwa kutoa ngoma kali bali pia yamekuwa yakimpongeza msanii huyo kuondoka kwenye lebo yake ya WCB.:

tunda_.tz

Richi the boss boy from tz waachee haoo waambiee kwann kifesi aliondok ukoo richi big up sana mzazi bora umetoka ukoo mpk hit song zako kidogo zipotee daaah komaa boss

_miss._.gucci

Hongera sana broo kwa kutoka WCB umefnya vzri broo nilishangaaa sana kukuona umeingia WCB coz uko n kipaji n sauti nzri zaidi ya dai sasa wameona unakuja vzri wameona gere ndugu yangu ww unaweza hata ukiwa nnje ya WCB so ss ma funz wko tunaomba uwaoneshe km unaweza n sio dai ndo alikua anakufanya usikike n upendwe ila n mungu n sio dai alikua anakufnya upende ila n mungu soo weka mungu mbele n evry thng gona be ok kwako soo pambana ss bdo tupo n ww wacha nao hao ma funz wko tunataka uzidshe bidii iliwapate tabu sanaaaa.

mussawaleo

ulinifanya niipende WCB N.a. umenifanya niichukie.

mr_misifa_2

NIMEFURAH UMETOKA UTUMWANI MWA FARAO WA WACLEAN, UKISIMAMA MWENYEWE UNAWEZA PIA NASHUKURU UMENITOLEA KUFULI

bishoo_la_instaa

Nyie mnao jifanya kumsifia mavoko niwa nafki na mna chuki na seemu aliyo kuepo mavoko kwasababu mavoko akuitwagwa #wcb bali alijiletaga mwenyewe(kama alivyo semaga kwenye interview) kuna watu wanadai(walitaka kumpoza,wengine kuusu ushirikina……na mambo mengine) kwanza mavoko kabla ajawa #wcb kawaida yake alikua nimtu wakimya kwenye mitandao unaweza uka fatilia intagram yake na you tube apost post sana sasa mnawezaje kudai ilipoingia #wcb ndo alikua kimya wakati ni kawaida yake tangu ajawa #wcb (kujitia mna mshabikia na amujui tabiya yake #mnachukinawcb mnaongea sana ila siku azigandi.

s.o.l.o.m.o.n_@yohan_aofficial

hajaona mafanikio ndo maana katoka! I this we was doing waaaay batter alivyokuwa mwenyewe! Hamna msanii asiependa mafanikio, that’s what I believe.

s.o.l.o.m.o.n_@kemieeeee

this is what I was telling people! The guy was diamond competitor! His music was so strong to stand as an independent artist, wasafi made him look like underground, depending on his boss! I hope he will continue making amazing music as he was before joining wasafi! I wish him lucky too.

wcb_4lif
@richmavoko unayumba #happy nyimbo mbaya kusema kweli tatz umetoka wasafi alf wewe unaonekana una matatizo ukai na watu vizur ilila papaa misifa alisema mavoko snichi na @diamondplatnumz auto muweza na ndio haya tunaona ila nyimbo yako mbovu na haifiki popote utaona.

Anyways tunaweza kusema maoni hayo ya mashabiki hayana uhalisia lakini je, kwa idadi ya watu hao wote ni kweli wanalolisema halina ukweli?

Na ni kwanini mashabiki wanamtangazia Rich Mavoko kuondoka WCB ile hali uongozi wa WCB na hata wasanii wenzake kutoka WCB wanakataa kuwa hajaondoka WCB?


Hii inatia hofu zaidi kwa Rich Mavoko kwani hata mfumo wa Q Boy msafi na Kifesi ulikuwa hivyo hivyo kuondoka WCB kila mtu alikataa kuwa hawana tofauti mpaka walipoamua wenyewe kufunguka.

Je, Rich Mavoko na wewe unasubiri hadi mashabiki wako wakushambulie mitandaoni ndio uje uongee? kwanini usiliweke wazi suala hilo kama ulivyoweka wazi wakati ule unasainiwa WCB.

Wahenga wanasema mficha maradhi kifo humuumbua, na ili uweze kuwa huru ni lazima uwaweke wazi mashabiki wako juu ya hatma yako ndani ya WCB hii itakufanya hata kama ni kweli umeondoka WCB uendelee kupendwa na mashabiki wako uliowavuna ukiwa WCB kwa miaka miwili.

Hebu fikiria shabiki wako wa WCB ambaye alizoea kuona kwenye BIO zako za mitandao ya kijamii umeweka lebo ya WCB lakini kwa sasa umefuta unadhani anapata picha nzuri kutoka kwako? bila shaka atakuchukia ni bora uwaweke wazi mashabiki wako.

 Mbaya zaidi Rich Mavoko kaachiwa wimbo wake mpya wa ‘Happy’ na wengi tumezoea kuona umoja wa WCB pale mmojawao anapoachia ngoma lakini wimbo huo hakuna msanii yeyote kutoka WCB wala kiongozi kuuposti kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Lisemwalo lipo na kama halipo laja pia Rich Mavoko kumbuka kuwa ni kawaida sana msanii kuondoka kwenye lebo yeyote ile na wala haiwagi siri kwa sababu muda una tabia ya kuhukumu.

Hata hao unaowaona akina Wizkid, Lil Wayne na wengineo wasanii wakubwa duniani wameshawahi kutemwa wengine kuondoka kwa sababu zao na walitangaza hadharani na kuweka wazi sababu zao na hadi leo wanapeta.

Tetesi za Rich Mavoko kuondoka WCB zilianza kusambaa tangu mwezi Juni lakini mpaka sasa uongozi wa WCB na wasanii wenzake wamekuwa wakidai wapo pamoja huku mwenyewe akikataa kabisa kuzungumzia ishu hiyo.

No comments:

Post a Comment