WILLIAN VS BARCELONA, MOURINHO NA WOORDWARD: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 23 July 2018

WILLIAN VS BARCELONA, MOURINHO NA WOORDWARD: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU


Chelsea wanatafakari iwapo wakubali kumuuza kiungo wao wa kati Mbrazil Willian kwa £65m kwa Barcelona, huku taarifa zikidokeza kwamba Manchester United pia wanataka sana kumnunua mchezaji huyo wa miaka 29. (Mail)

Klabu hiyo ya Stamford Bridge inadaiwa pia kuwa katika juhudi za kutafuta eneo salama uwanjani ambapo kocha wao mpya Maurizio Sarri, 58, anaweza kuwa akivutia sigara hata siku ya mechi. Sarri ni mvutaji sugu wa sigara. (Mirror)

Chelsea pia wanaaminika kuwa bado na matamanio ya kumnunua mshambuliaji Mfaransa anayechezea Manchester United Anthony Martial, 22. (Talksport)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anatarajiwa kukutana na makamu mwenyekiti mtendaji wa klabu hiyo Ed Woodward kujadiliana kuhusu wachezaji watakaonunuliwa au kuuzwa na klabu hiyo. (Express)

Beki wa Argentina Marcos Rojo, 28, ndiye mchezaji anayetarajiwa na wengi kuoneshwa lango ikiwa United watafanikiwa kumnunua beki wa England Harry Maguire, 25, kutoka Leicester. (Mirror)

Uwezekano wa Liverpool kumnunua kiungo wa kati wa Lyon Nabil Fekir, 25, unaonekana kufifia baada ya madai kuibuka kwamba huenda kusiwe na maafikiano. (Express)


Hata hivyo, klabu hiyo ya Anfield inadaiwa kuwa kwenye mazungumzo na klabu ya Besiktas ya Uturuki kuhusu uwezekano wa kumchukua beki wa Croatia Domagoj Vida, 29. (Star)

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment