Wezi waiba gari na mtoto wa mwezi mmoja akiwa ndani - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 20 July 2018

Wezi waiba gari na mtoto wa mwezi mmoja akiwa ndani

Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Claire O’Neill amejikutana akiungana kwa mara nyingine na mtoto wake wakike wa miezi minne baada ya wezi kuiba gari lake likiwa na mwanae huyo ndani.

Claire O’Neill mwenye umri wa miaka  39, raia wa Uingereza alimuacha mtoto huyo kwenye gari lake aina ya ‘Audi A3 sports’ nje ya nyumba yake huko Birmingham kabla ya wezi kuliiba hapo jana siku ya Alhamisi majira ya mchana.
Wezi hao waliyokadiriwa kuwa wawili walikuwa wakimfuatilia mama huyo aliyekuwa amempakia mwanae kichanga anayejulikana kwa jina la Eliza kwenye siti za gari hiyo.
Majirani wa karibu wamesema kuwa wamesikia mama huyo akipiga kelele akisema ”mtoto wangu”, ”mtoto wangu” kisha gari kukipimbia.
Baada ya operesheni ya jeshi la polisi alikutwa mtoto huyo akiwa ameachwa kwenye kituo cha ‘health centre’ kabla ya kurudishwa kwa mama yake ambaye ameonekana kuvuja damu baada ya tukio hilo. 
Mapema hii leo polisi waliweka hadharani picha zinazo muonyesha mama huyo akiwa na mwanae  hospitali.
Majirani na marafiki wa karibu wamemtumia salamu nyingi za kumtakia gheri kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii.

Tukio hili linajiri baada ya kupita siku tatu pekee kutokea kwa tukio kama hilo la wizi wa aina ya gari ya Audi S3 maili sita kutoka Nechells.

No comments:

Post a Comment