Wengi washuhudia kupatwa kwa mwezi - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 28 July 2018

Wengi washuhudia kupatwa kwa mwezi

Mamilioni ya watu duniani wameshuhudia tukio la kihistoria la kupatwa kamili kwa mwezi. Tukio hilo la muda mrefu zaidi katika karne hii limeshuhudiwa usiku wa kuamkia leo wa Julai 27 mwaka 2018 huku nchini Tanzani na Barani Afrika kwa ujumla, Australia, Asia, Ulaya na Amerika Kusini.
Kupatwa huko kwa mwezi kumedumu kwa takriban saa 1 : 43  huku tukio zima likidumu kwa karibu masaa manne. Nchini Somalia, baadhi ya watu walikimbilia misikitini kwa ajili ya sala maalumu ambayo hufanywa wakati wa tukio hilo.
Nchini Sudan Kusini watu walijaribu kupiga picha ingawa upigaji wa picha kwa kutumia kamera huzuiwa nchini humo. Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia pia umelishuhudia vizuri tukio hilo wakati ikiwa katika majira ya mvua.
Amerika ya Kaskazini hawakufanikiwa kushuhudiwa tukio hilo la jana usiku lakini wakitarajiwa kuliona lile litakalotokea Januari 21, 2019, hii ikiwa ni kulingana na taasisi ya masuala ya anga ya Marekani NASA.

No comments:

Post a Comment