Video: Diamond apokewa kifalme Mayotte, akabidhiwa mrembo - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 28 July 2018

Video: Diamond apokewa kifalme Mayotte, akabidhiwa mrembo

Msanii wa muziki na rais wa WCB, Diamond Platnumz amepokewa kama mfalme katika kisiwa cha Mayotte ambapo anatarajia kufanya show ya nguvu weekend hii baada ya kumaliza tour yake ya Marekani.

Muimbaji huyo muda mchache baada ya kupokewa na burudani za ngoma na kupewa zawadi, aliondoka kuelekea kwa wenyeji wake huku akiwa na mrembo ambaye alipanda naye gari moja.
“HANK YOU MAYOTTE!!! YOU GUYS MADE ME FEEL LIKE , AM AT HOME!!! I CAN’T WAIT TO PARTY WITH TOU TONIGHT!!!🙏🏻,” aliandika Diamond.
Mapema wakati yupo njiani kuelekea Mayotte, alipitia Madagascar na kuona namna gani mashabiki wanavyomkubali.
“Kabla ya show yangu nitayoifanya Madagascar tareh 4/ 08…juzi nilipita nikalala siku moja kisha nikaunga ndege kuja Mayotte…ulalaji wangu pale nilijifunza na nilistaajabishwa na vingi, Kwanza kabisa asilimia kubwa ya watu wa Madagascar ni kama wachina walomix na Wahindi, halaf wanalugha yao pekeyao, kisha Kifaransa ndio Lugha yao ya pili….kilichoniataajabisha ni kwamba wamenijuaje sasa,” aliandika Diamond.

No comments:

Post a Comment