Usajili uliotia fora zaidi, watambulishwa kwa ‘helicopter’ jiji lazizima (+Picha) - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 21 July 2018

Usajili uliotia fora zaidi, watambulishwa kwa ‘helicopter’ jiji lazizima (+Picha)

Mapema juzi siku ya Alhamisi klabu ya Feyenoord inayoshiriki ligi ya Uholanzi imesherehekea miaka 110 ya kuanzishwa kwake huku ikiwatambulisha wachezaji wake wapya wawili.
Katika sherehe hizo wachezaji, Yassin Ayoub na Luis Sinisterra ambao ni wapya walipata bahati ya kutua na ‘helicopter’ ndani ya uwanja wa klabu hiyo na kutambulishwa mbele ya washabiki waliyohudhuria sherehe hizo.
Maelfu ya washabiki walijitokeza kushuhudia historia hiyo ya klabu ya Rotterdam ambayo imeshinda jumla ya mataji 15 ya ligi ya Eredivisie huku la mwisho ilikiwa msimu wa mwaka 2016/17.
Mchezaji raia wa Moroco, Ayoub (kushoto) na Sinisterra wakitambulishwa 
Wachezaji hao wapya  Ayoub na Sinisterra wametua kwa mbwembwe dimba la De Kuip huku wakipokelewa na mziki mzito kutoka kwa DJ Afrojack.
Maelfu ya mashabiki wakiwa wamejitokeza kwenye sherehe hizo
Robin van Persie ni miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo waliyo hudhuria sherehe hizo huku wakitambulisha jezi zao mpya za msimu huu.
Robin van Persie akisaini jezi za mashabiki
DJ Afrojack raia wa Uholanzi akiburudisha

No comments:

Post a Comment