UONGOZI WA JUU YANGA WAKUTANA NA WACHEZAJI KUTATUA TATIZO LA MGOMO - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 22 July 2018

UONGOZI WA JUU YANGA WAKUTANA NA WACHEZAJI KUTATUA TATIZO LA MGOMO


Viongozi wa Yanga wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti Clement Sanga, leo mchana huu wanakutana na wachezaji wa klabu hiyo kwa ajili ya kujadili matatizo mbalimbali yanayokumba wachezaji wake.

Sanga atakuwa na viongozi mbalimbali kutoka Kamati ya Mashindano ya Yanga wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Hussein Nyika, kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo madai ya wachezaji.

Ijumaa ya wiki hii wachezaji wa Yanga waligoma kufanya mazoezi ambapo Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera alijikuta akiwa na wachezaji watano pekee kutokana na kudai stahiki zao ikiwemo fedha za mishahara.

Sanga kwa kushirikiana na Kamati ya Mashindano wamemua kuitisha kikao maalum ili kumaliza suala hilo likiwemo pia la kuowaongezea mikataba wachezaji ambao bado hawajamalizana na Yanga ikwemo Beno Kakolanya na Hassan Kessy.

Wachezaji wa Yanga waliingia kwenye mgomo wa mazoezi zikiwa ni siku kadhaa tangu wacheze mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia na wakati huo wanapaswa kuanza maandalizi kuelekea mechi ya marudiano itakayopigwa Julai 29 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment