Tetesi za Barnaba Kurudiana Kimapenzi na Mama Steve, Ukweli Huu Hapa - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 30 July 2018

Tetesi za Barnaba Kurudiana Kimapenzi na Mama Steve, Ukweli Huu Hapa

Mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Chausiku’ Barnaba Boy Classic, Zubeda amekataa kabisa Kurudisha Penzi kwa Baba watoto wake huyo.

Zubeda na Barnaba walikuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kwa miaka mingi na hata kujaaliwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume lakini penzi lao lilivunjika na kila mmoja kushika njia yake.

Siku chache zilizopita kulikuwa kuna tetesi kuwa wawili hao wameweka tofauti zao pembeni na kuamua kuwa pamoja tetesi ambazo Zubeda amezikataa na kudai hawezi kurudi kwa mzazi mwenziye kwa sababu kila mtu ana maisha yake mengine.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Zubeda alisema kila mtu kwa sasa yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaheshimiana katika hilo kilichobaki kwao kubaki kama wazazi na hakuna lingine zaidi ya hilo kwa sababu tangu wametengana ni muda mrefu sasa.

Watu wanadai tu kuwa nimerudi kwa Barnaba, lakini sio kweli kabisa yule ni mzazi mwenzagu tu na ataendelea kuwa hivyo na si kitu kingine kwa sababu nina mtu wangu na yeye ana mtu wake kilichobaki ni heshima tu ya mzazi mwenzangu”.

No comments:

Post a Comment