Suala la kuachana na mama watoto wangu Tessy linaniuma sana – Aslay - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 23 July 2018

Suala la kuachana na mama watoto wangu Tessy linaniuma sana – Aslay

Msanii wa muziki, Aslay aka Baba Moza amedai kwamba hapendi kulizungumzia suala la kuachana na mama watoto wake, Tessy.
Wawili hawa wamefanikiwa kupata mtoto mmoja, Moza lakini kwa sasa hali imechafuka huku Aslay akidaiwa kuhamishia majeshi kwa msanii wa filamu Diana Kimario.
“Huwa sipendi kulizungumzia hili suala kwa sababu linaniumiza sana, ila ukweli ndio huo kama ulivyosikia nimeachana na mama Moza,” Aslay aliliambia Gazeti la Mwanaspoti.
Aliongeza, “Ni mambo ya familia na kilichobaki kwa sasa ni uhusiano wa wazazi wenye mtoto, ambaye anahitaji uangalizi wa pande zote. Unajua kuna baadhi ya watu wanadhani kuwa hii ni kiki, lakini mimi sio mtu wa kiki kabisa na ninazungumza hapa ni ukweli mtupu,”
Kwa sasa Tessy anadaiwa kuangukia kwenye mikono ya bonge la bwana mmoja hapa jijini huku muimbaji huyo akidaiwa kutoka na muigizaji Diana Kimaro.

No comments:

Post a Comment