Sitaki Kuona Simu Magerezani kwa Wafungwa na Chakula Wajilishe Wenyewe- Lugola - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 21 July 2018

Sitaki Kuona Simu Magerezani kwa Wafungwa na Chakula Wajilishe Wenyewe- Lugola

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amemtaka Mkuu wa Magereza nchini, Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Martin Kasike,  kuweka na kumpelekea mikakati ya kuhakikisha wafungwa wanajilisha kwa kufanya kazi badala ya kulishwa kwa fedha za serikali.

Ameonya pia kwamba iwapo mfungwa atakamatwa na simu gerezani, mkuu wa gereza husika atakuwa amepoteza sifa za kazi yake.

Lugola ameyasema hayo leo  alipozungumza na vyombo vya habari na kusisitiza wito wa Rais John Magufuli wa kutaka wafungwa wajitegemee kwa chakula na kuhakikisha wafungwa hawaingizi simu gerezani.

“Nimemuelekeza Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini kutengeneza mkakati maalum kuhakikisha wafungwa wote nchini wanajilisha kuanzia mboga, kama ni kufuga samaki au kulima maharage, na kusiwe na kisingizio chochote kwani jambo hili linatekelezeka,” alisema.
Alisema bunge lijalo litaanza kubadilisha sheria ili kusiwe na kinga kwa wafungwa ili wafanye kazi, wajilishe na wawalishe mahabusu, na ikiwezekana magereza yazalishe chakula cha ziada kwa kuuza na kutengeneza kipato.

No comments:

Post a Comment