Simba ya Mwaka Huu si Mchezo, Lazima Wachukue Kombe Tena - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 29 July 2018

Simba ya Mwaka Huu si Mchezo, Lazima Wachukue Kombe TenaWakati kikosi cha Simba kikiwa katika programu ya mazoezi nchini Uturuki kwa takribani wiki moja sasa, uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa Kocha Msaidizi, Masoud Djuma, umesema timu hiyo haitoshikika msimu ujao. 

Simba ipo Instabul katika Milima ya Kartepe ikijifua kwa maandalizi ya tamasha la Simba Day ambalo khufanyika Agosti 8 kila mwaka pamoja na msimu mpya ujao wa Ligi Kuu Bara. 

Taarifa zimeeleza Djuma amesema kila mchezaji ameahidi makubwa kuelekea pazia la ligi kufunguliwa ambapo Simba itaanza kucheza dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Aidha, Kocha huyo amefunguka na kusema uwepo wa Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems umechangia kwa wachezaji wote kujituma zaidi mazoezini ili kumuonesha uwezo walionao. 

Mbali na programu za mazoezi, kikosi cha Simba kimekuwa kikiingia darasani kupewa mafunzo mbalimbali ili kuwaongezea uelewa wachezaji wake ikiwemo elimu ya saikolojia. 

Baada ya kambi hiyo kumalizika, SImba wataanza kurejea jijini Dar es Salaam Agosti 4 tayari kwa maandalizi ya Simba Day na mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Suhar utakaopigwa Agosti 12 Uwanja wa CCM Kirumba.

No comments:

Post a Comment