Simba SC yamsajili Kiungo Mzambia Cletus - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 22 July 2018

Simba SC yamsajili Kiungo Mzambia Cletus


Klabu ya soka nchini Simba SC inaendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao, baada ya kumsajili kiungo mshambuliaji, Mzambia Cletus Chama Chota kutoka Lusaka Dynamos.

Chama ambaye alikuwa Nahodha wa Lusaka Dynamos ametambulishwa leo na Rais wa Klabu, Salim Abdallah ‘Try Again’ mbele ya kocha mpya, Mbelgiji Patrick J Aussems.

Chama anakuwa mchezaji mpya wa tatu wa kigeni, baada ya beki mu-Ivory Coast, Serge Wawa Pascal na mshambuliaji kutoka Rwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere.

Pamoja na Dynamos, timu nyingine alizowahi kuchezea Chama mwenye umri wa miaka 27 sasa ni Ittehad ya Misri, ZESCO United FC na Nchanga Rangers FC za huko Zambia.

Pia wanaungana na Waghana, beki Asante Kwasi , kiungo James Kotei na mshambuliaji Nicholas Gyan, Waganda Emmanuel Okwi, Juuko Murshid, Mrundi Laudit Mavugo na Mnyarwanda Haruna Niyonzima.

No comments:

Post a Comment