Sasa Ninja Nimeingia Mawaziri Wote Waliopita Hawakuwa Maninja- Lugola - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 22 July 2018

Sasa Ninja Nimeingia Mawaziri Wote Waliopita Hawakuwa Maninja- Lugola

Waziri wa mambo ya ndani Kagi Lugola amesema kuwa mawaziri wote wa mambo ya ndani waliopita hawakuwa maninja na sasa ameingia Ninja ambaye ndio yeye.Maneno hayo ameyaongea katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam wakati akitoa Tathimini ya ziara zake alizozifanya kuanzia Julai 11 2018 katika miongoni mwa taasisi zilizochini ya wizara yake ya Mambo ya ndani.

Wakari anaongea ameweza kuongea mambo kibao likiwemo la kumuagiza mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Vitambulisho vya taifa (NIDA) Andrew Massawe kufika ofisini kwake katika ofisi zake za Dodoma, afike pamoja na mtambo wa kutengenezea Vitambulisho vya taifa.Lakini pia Waziri Lugola ameweza kutoa tamko la kumwagiza mkuu wa polisi nchini Saimon Siro kumpeleka Lugumi ofisini kwake Mnamo Julai 31 mwaka huu Jijini Dodoma haraka iwezekanavyo.Waziri Lugola ameongeza kuwa angependa kuona Lugumi anafika ofisini kwake asubuhi pale anaposikia habari hizi “Ntapenda kuona anafika ofisini kwangu agonge mlango ninaposema karibu nikifungua mlango nimkute ni yeye sio lazima mpaka afuatwe na polisi kwa Lugumi ana  familia na anaishi Tanzania”

No comments:

Post a Comment