Real Madrid kuanza ligi bila mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 28 July 2018

Real Madrid kuanza ligi bila mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or

Klabu ya Real Madrid kwa jina la utani wakijulikana kama Los Blancos kutoka nchini Uhispania, ambao ni mabingwa wa mara 33 wa ligi hiyo pia washindi wa mara 13 wa ligi ya mbaingwa barani ulaya UEFA.
Kwa mara ya kwanza tangu Florentino Perez awe rais wa klabu hiyo wanatarajia kuanza msimu mpya wa ligi 2018/2019 bila kuwa na mchezaji yeyote ambaye alishawahi kushinda tuzo ya Ballon d;Or.
Hali hii iliyowatokea mabingwa hawa wa UEFA ilishawahi kuwatokea miaka 18 iliyopita nikimaanisha mara ya mwisho kutokewa na hali hii ilikuwa ni mwaka 2000 ambapo timu ilianza ligi bila kuwa na mchezaji aliyeshinda tuzo ya Ballon d’or.ambapo mwaka huo walimnunua Luis Figo kutoka kwa wapinzani wao wakubwa FC Barcelona kwa uhamisho uliovunja rekodi wa Euro mil 37.
Real Madrid wametokewa na hali hiyo baada ya kumuuza mchezaji wao aliyeshinda Tuzo hiyo kwa nyakati tano tofauti ambaye amejiunga na Mabibi kizee wa Turin Juventus,huyo sio mwingine bali ni Cristiano Ronaldo.
Kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 18 klabu hiyo inaanza ligi bila kuwa na mchezaji aliyeshinda tuzo hiyo kubwa kabisa duniani,tangu Alfredo Di Stefano alivyoondoka mwaka 1964. wachezaji kama Zidane, Figo walikuja kurudisha heshima ya klabu hiyo.
Hawa ndio washindi wa tuzo ya Ballon d’Or kutoka Real Madrid,lakini kuna msimu hakuna mshindi katika klabu hiyo lakini mchezaji aliyeshinda tuzo lazima apatikane angalau hata mmoja.
Mfano mwaka ambao Messi anashinda tuzo Ronaldo alikuwepo Real Madrid lakini mwaka huu hakuna hata mchezaji mmoja ambaye alishawahi kushinda tuzo hiy.
Ndani ya miaka 18 ambayo walishinda wachezaji wa Real Madrid na hii ndio Orodha ya washindi hao.
2000-01: Luis Figo
2001-02: Luis Figo, Zinedine Zidane (2002), Ronaldo (1997, 2002)
2002-03: Luis Figo, Zinedine Zidane, Ronaldo
2003-04: Luis Figo, Zinedine Zidane, Ronaldo
2004-05: Zinedine Zidane, Ronaldo, Michael Owen (2001)
2005-06: Zinedine Zidane, Ronaldo
2006-07: Fabio Cannavaro (2006, Ronaldo
2007-08: Fabio Cannavaro
2008-09: Fabio Cannavaro
2009-10: Kaka (2007), Cristiano Ronaldo (2008)
2010-11: Kaka, Cristiano Ronaldo
2011-12: Kaka, Cristiano Ronaldo
2012-13: Kaka, Cristiano Ronaldo
2013-14: Cristiano Ronaldo (2008, 2013)
2014-15: Cristiano Ronaldo (2008, 2013, 2014)
2015-16: Cristiano Ronaldo
2016-17: Cristiano Ronaldo (2008, 2013, 2014, 2016)
2017-18: Cristiano Ronaldo (2008, 2013, 2014, 2016, 2017)
By Ally Juma.

No comments:

Post a Comment