RASTA WA HANSPOPE ATUA SINGIDA UNITED - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 25 July 2018

RASTA WA HANSPOPE ATUA SINGIDA UNITED


Singida United imezidi kufukuzana na masaa kuelekea kufungwa kwa dirisha la usajili kesho kabla ya saa sita kwa kuingia mkatana na mchezaji Awesu Ally wa miaka miwili.

Ally ambaye aliwahi kuichezea Mwadui FC, amefikia makubalino na mabosi wa Singida kwa kutia kandarasi hiyo tayari kukipiga na walima alizeti hao.

Kiungo huyo ambaye aliwahi kumvutia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hanspope, inawezekana akawa sehemu ya kukamilisha idadi ya wachezaji wapya ndani ya Singida United.

Pope alikutana na Ally wakati kikosi cha Simba kiliposafiri miaka kadhaa nyuma kuelekea Arusha kwa ajili ya mechi ya kirafiki na kufanikiwa kukutana na mchezaji huyo kisha baadaye kuripotiwa kuwa timu hiyo inamhitaji mchezaji huyo.

Baada ya Singida kukamilisha usajili huo, Shirikisho la Soka nchini (TFF) limezidi kusisitiza kuwa halitaweza kuongeza siku za usajili baada ya kesho, Julai 26 2018.

No comments:

Post a Comment