RASMI SIMBA YAINGIA MKATABA WA MIAKA MIWILI NA KIUNGO MZAMBIA - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 22 July 2018

RASMI SIMBA YAINGIA MKATABA WA MIAKA MIWILI NA KIUNGO MZAMBIA


Rasmi klabu ya Simba imeingia mkataba wa miaka miwili na kiungo Mzambia, Chama Clatous kutoka Dynamo FC.

Simba wamefikia makubalino na mchezaji huyo ambaye sasa atakuwa kwenye msafara wa kikosi cha timu hiyo kitakachoelekea Uturuki leo kwa kambi maalum kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Clatous ametua Simba ili kuongeza nguvu katika idara ya kiungo ambapo sasa atakuwa pamoja na wachezaji wengine kama Shiza Kichuya na Jonas Mkude.

Simba wamezidi kukiboresha kikosi chao zikiwa zimesalia siku 4 pekee kuelekea kufungwa kwa dirisha la usajili kwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment