RAIS WA ZANZIBA DK.ALI MOHAMED SHEIN AWASILI NCHINI INDONESIA LEO. - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 31 July 2018

RAIS WA ZANZIBA DK.ALI MOHAMED SHEIN AWASILI NCHINI INDONESIA LEO.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt Ramadhani Kitwana Dau (kulia) mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta Indonesia leo, akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Viongozi mbali mbali,katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla,[Picha na Ikulu.]31/07/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt Ramadhani Kitwana Dau,mara baada ya mapokezi alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta Indonesia leo  akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kushoto)  pamoja na Viongozi mbali mbali, katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla ,[Picha na Ikulu.]31/07/2018.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt Ramadhani Kitwana Dau (kulia)  na Viongozi wengine wakipewa maelekezo na Afisa Maalum mara baada ya  mapokezi walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta Indonesia leo wakiungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ziara ya siku saba Nchini humo kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla ,  [Picha na Ikulu.]31/07/2018. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kiongozi wa Ngazi ya Juu Nchini Indonesia Daniel T.S.Simanjuntak (kushoto) mara alipowasili katika Ukumbi wa Watu Mashuhuri katika Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta leo, akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Viongozi mbali mbali,katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla ,[Picha na Ikulu.]31/07/2018.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe  Mama Mwanamwema Shein (katikati) wakibadilishana mawazo na  Kiongozi wa Ngazi ya Juu Nchini Indonesia Daniel T.S.Simanjuntak (kulia) katika Ukumbi wa Watu Mashuhuri katika Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta leo mara baada ya mapokezi yake  katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla,(kushoto) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt Ramadhani Kitwana Dau, [Picha na Ikulu.]31/07/2018. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe  Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na Viongozi aliofuatana nao akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Ngazi ya Juu Nchini Indonesia Daniel T.S.Simanjuntak (wa pili kulia)  katika Ukumbi wa Watu Mashuhuri katika Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakartaleo katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchini Indonesia Mhe.Mohammed Jusuf Kalla, [Picha na Ikulu.]31/07/2018.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe  Mama Mwanamwema Shein wakipokea mashada ya mauwa mara walipowasili katika Viwanja vya Borobudur Hotel Jakarta Nchini Indonesia leo  
katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchini Indonesia Mhe.Mohammed Jusuf Kalla, [Picha na Ikulu.]31/07/2018.  
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewasili nchini Indonesia leo kwa ajili ya ziara maalum ya kikazi kufuatia mwaliko wa Makamo wa Rais wa nchi hiyo Muhammad Jusuf Kalla. 
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Indonesia, Soekarno- Hatta, uliopo mjini Jakarta Dk. Shein alipokelewa na miongoni mwa viongozi wakuu wa Serikali wa Nchi pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia ambaye pia anaiwakilisha nchi hiyo Ramadhan Dau.
Ziara hiyo ya Dk. Shein ambayo inatarajiwa  kuanza rasmi hapo kesho itaanza kwa  mazungumzo na mwenyeji wake Makamo wa Rais wa nchi hiyo Muhammad Jusuf Kalla na baadae kufanya mazungumzo na viongozi wengine mbali mbali wa ngazi za juu wa Serikali pamoja na viongozi wa sekta binafsi wa nchi hiyo. 
Katika ziara hiyo, Rais Dk. Shein amefuatana na viongozi mbali mbali akiwemo Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Balozi Amina Salum Ali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa, Haji Ussi Gavu, na viongozi wengine wa Serikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kufanya ziara nchini humo ambayo atakutana na viongozi wakuu, kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, kukutana na wafanyabiashara, kutembelea sehemu za utamaduni na zile za kitalii.
Dk. Shein anatarajiwa kurejea nchi Agosti 6, mwaka huu.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

No comments:

Post a Comment